Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mchengerwa (Mb) leo tarehe 16/09/20203 amewaambia wananchi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba kuwa serikali italeta watumishi 76 wa kada za afya na elimu ili kukidhi mahitaji yaliyopo. Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Mhe. Abdallah Dadi Chikota kumueleza Raisi Samia kuwa pamoja na jitihada kubwa za serikali ya awamu ya sita kuboresha sekta ya elimu na afya kwa kujenga shule na hospitali za kisasa lakini bado Halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi katika sekta hizo.
Rais Samia Suluhu leo alisimama katika eneo la Mahakamani, Halmashauri ya Mji Nanyamba kusalimia mamia ya wananchi waliojitokeza kumlaki wakati akiendelea na ziara za kikazi katika mkoa wa Mtwara. Katika salam hizo, Mhe. Rais aliwataka wananchi kutumia vizuri miradi ya maendelo inayopelekwa katika Halmashauri hiyo ikiwemo kiwanda cha kubangua korosho kinachotarajiwa kujengwa eneo la Maranje ili kujipatia mafanikio kiuchumi na kijamii.
Katika hatua nyingine, Mhe. Raisi aliwataka wananchi hao kuitumia vizuri shule mpya ya ya wasichana kidato cha tano na sita kwa kuwapeleka watoto wa kike shule. Rais Samia pia aliongeza kwa kusema “Ni mpango wa serikali kuwa kila mkoa uwe na shule kubwa ya wasichana kwa mchepuo wa sayansi, na hapa Mtwara hivi karibuni itaanza kujengwa”.
Katika kuthibitisha ule usemi “Mgeni njoo, mwenyeji apone” Mbunge wa Nanyamba Mhe. Chikota alimuomba Mhe. Rais kuweza kuongeza bei ya zao la korosho ili wakulima waweze kunufaika na zao kwani ndilo zao la biashara wanalotegemeabkwa ustawi wa uchumi.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.