Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Mji Nanyamba Kwa kushirikiana na Diwani wa kata ya Hinju, Mhe. Rashid Mohamed Ngongo pamoja na wananchi wa kata hiyo wameshiriki shughuli za ujenzi wa shule ya sekondari Hinju.Shule ya sekondari Hinju ni miongoni mwa shule itakayokamilisha mpango wa serikali wa kila kata kuwa na shule ya kata. Mara baada ya ujenzi kukamilika tarehe 29/02/2024 Shule inatarajia kupokea wanafunzi 82 wa Kidato cha kwanza ambapo wavulana ni 35 na wasichana ni 47.
Umalizikaji wa shule hiyo kutasaidia kutatua changamoto ya wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kusoma shule ya sekondari Njengwa.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.