Mwenge wa Uhuru 2024 unatarajiwa kupokelewa Halmashauri ya Mji Nanyamba katika viwanja vya shule ya msingi Maranje siku ya Jumamosi tarehe 01/06/2024 ukitokea Hamashauri ya wilaya ya Mtwara kabla ya kuelekea Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba. Ukiwa Halmashauri ya Mji Nanyamba Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya Bilioni 7.73 (7,734,017,196.34) za kitanzania.
Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni Pamoja na; Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Maranje; Shamba la Miti lenye hekari 10 katika Kijiji cha Chawi; Uwashwaji wa Umeme (REA) katika Kijiji cha Chawi; Uendelezaji wa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mkomo; Ujenzi wa Barabara ya lami yenye urefu wa kilometa moja iliyopo mtaa wa Kilimanjaro; Kikundi cha vijana Pambamoto Pamoja na ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Umoja kilichopo kata ya Milangominne.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni “Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu”.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.